Mradi wa kuimarisha mifumo katika sekta za umma (PSE) umeendesha mafunzo ya siku mbili kwa waheshimiwa madiwani wa Mkoa wa Mbeya tarehe 11 Mei 2017 na tarehe 12 Mei 2017. Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Paul Ntinika akimwakilisa Mkuu wa Mkoa Mh. Amos Makalla amewataka Waheshimiwa Madiwani kutumia mafunzo elekezi hayo kama yalivyokusudiwa kwa kuhakikisha wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizo.
Pia Mh. Ntinika amewashukuru wafadhili wa mradi huo kuleta mafunzo hayo katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kwani mafunzo hayo yanalenga kuinua uwajibikaji kwa waheshimiwa madiwani ili wawasimamie vizuri wataalamu katika kuwatumikia wananchi.
Naye Mh. Mwalingo Kisemba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya amesema kuwa wao kama Waheshimiwa Madiwani wamenufaika na mafunzo hayo kwani yamewaongezea mbinu na maarifa katika kusimamia miradi ya maendeleo na pia yamewasaidia kuelewa mipaka yao kwa mujibu wa kanuni, taatibu na sheria zilizopo.
Pia Mh. Kisemba ametoa rai kwa serikali kuwa ni vyema mafunzo haya yakawa endelevu kwani kwa mujibu wa sheria udiwani unakoma kila baada ya miaka mitano. Na akashauri kwa awamu ijayo yaani mwaka 2020 ni vyema mafunzo hayo yakatolewea punde tu waheshimiwa madiwani wanapoapishwa ili wasipate tabu katika kutekeleza majukumu yao.
Mradi wa PS 3 unafadhiliwa na Watu wa Marekani chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo (USAID). Dr. Peter Kilima Mkurugenzi wa Mradi wa PS 3 amesema kuwa mradi huu ni mradi wa miaka mitano ambao umeanza kutekelezwa mwaka 2015 hadi mwaka 2020.
Pia Dr. Kilima amesema kuwa mradi huu unatekelezwa katika Halmashauzi za mikoa 13 ukiwemo mkoa wa Mbeya. Amesema pamoja na kazi nyingine za kuimarisha mifumo ya sekta ya umma pia mradi umelenga kuwajengea uwezo waheshimiwa madiwani ili waweze kuzisimamia ipasavyo Halmashauri zao.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.