MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA
Mwenge wa uhuru umekagua miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2 Halmashauri ya wilaya ya Mbeya tarehe 30.08.2024 na kiongozi wa Mwenge ndugu Godfrey Eliakim Mnzava.
Mwenge wa uhuru ulipokelewa katika viwanja vya Simambwe saa mbili asubuhi ukitokea Mbarali na kupokelewa na Katibu Tawala ndugu Mohammed Azizi Faki (DAS) ambapo ulikimbizwa kilomita 2227.2 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mwenge wa uhuru ulianza na kukagua mradi wa kwanza ambao ni mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya tarajiwa cha Igoma ambao ulianza kujengwa tarehe 15/02/2020 kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Mbeya. Wananchi wa Kata ya Igoma waliunda kamati za ujenzi, kuhamasishana kusogeza fursa kama mawe mchanga, tofali, kuchota maji, usafishaji wa eneo, kujenga msingi na kupandisha boma la jengo la upasuaji na kuliezeka kwa nguvu zao wenyewe, Michango hii ya nguvu kazi za wananchi inakadiriwa kuwa na thamani ya Tsh 34,470,500.00. Halmashauri katika kutambua jitihada hizi za wananchi ilitoa fedha kiasi cha Tsh 110,000,000 katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la Upasuaji kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri
Mwenge wa uhuru ulikagua pia mradi wa maji Simambwe wenye thamani ya shiling 488,913,979.00,Ambao utasambaza maji hayo katika sehemu zote za Kata ya Simambwe. Mradi huu unatumia chanzo cha Chem chem ya Salalani chenye uwezo wa lita 10.1 kwa sekunde
Aidha mwenge pia umekagua Msitu wa hifadhi Ikhoho, msitu huu umepakana na kata mbili za Maendeleo na Tembela ni msitu wa Serikali kuu unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Pia msitu huu una mito miwili (2) mikubwa ya Mlowo na Patagwa ambayo hupeleka maji yake mto Ruaha Mkuu na hatimaye maji yake kutiririka mpaka bwawa la Mwl. Nyerere.
Utunzaji wa bioanuai iliyopo (wanyama na mimea)-Msitu wa hifadhi Ikhoho una mimea na miti ya aina mbalimbali ambayo ipo hatarini kutoweka kama haitatunza vizuri, aidha kuna wanyama wadogo kama nyani, nyoka, ndege na wadudu wa aina mbalimbali; hivyo msitu huu ni makazi ya Wanyama na viumbe hai wengine.Hifadhi ya mazingira na utunzaji wa ardhi kwa ujumla.Msitu huu hurekebisha hali ya hewa na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.Msitu huu hutumika kwa matambiko ya kimila pamoja na dawa za asili.
|
|
|
Mkimbiza mwenge pia aliweka jiwe la msingi katika daraja la Imezu lenye urefu wa mita 7, upana wa mita 5.7 na kina cha Mita 4 katika barabara ya Imezu, Mradi huu umetokana na umuhimu katika jamii kwa kuwa ni Daraja pekee linalounganisha Wilaya ya Mbarali.
Ujenzi wa daraja la Imezu unagharamiwa na fedha za Matengenezo ya barabara kiasi cha TZS. 118,531,440.00 (Milioni Mia moja kumi na nane, mia tano thelathini na moja elfu na mia nne arobaini). Hadi sasa fedha iliyolipwa kwa Mkandarasi ni kiasi cha TZS. 82,420,040.00 sawa na 69.5% ya Mkataba wake. Kiasi cha fedha kilichoshikiliwa (Retention Money) kwa mujibu wa mkataba ambacho kitalipwa baada ya muda wa matazamio kuisha (Defect Liability Period) ni TZS. 8,242,004.00 ambayo itafanya jumla ya TZS. 95,647,720.00 sawa na (80.69%) ya kazi zote alizofanya.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inatoa huduma na fursa za kielimu kwa makundi maalum ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu wenye Ulemavu wa akili, Ulemavu wa viungo, albino, viziwi na wasioona na kufanya kuwa na jumla ya wanafunzi 585, wakiwemo Wavulana 331 na Wasichana 254.
Lengo la Serikali ni kuwapa fursa za Kielimu wanafunzi wenye mahitaji maalum na huduma nyingine za kijamii.
Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inatoa jumla ya Tshs 186,121,260.00 kila mwaka kwa ajili ya chakula cha Watoto wenye mahitaji maalum ikiwa ni Tshs 318,156.00 kwa kila mwanafunzi mwenye mahitaji maalum kwa wanafunzi 585. Aidha kiasi cha Tsh 4,230,000.00 kimetolewa kwenye fedha za Mchango wa mwenge kwa ajili ya kununua vifaa saidizi na vifaa vya kufundishia vikiwemo Viti mwendo, Mafuta ya kuzuia jua na kofia kwa ajili ya Watoto wenye ulemavu wa Ngozi, midoli, na shimesikio.
Pia mwenge wa uhuru umekagua kikundi cha vijana Gombe wanaojishughulisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki. Kikundi hiki kilianzishwa mwaka 2019 kikiwa na wanachama 16. Kwa sasa wamebaki vijana 8 wengine 8 wamekosa sifa ya kuendelea kuwa wanakikundi kutokana na kuzidi umri hivyo wamebaki kuwa washauri. Kikundi kinapatikana Kata ya Bonde la Songwe, kijiji cha Ikumbi, kitongoji cha Ifisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mtaji wa kikundi hiki ni kiasi cha Tshs. 49,500,000.00 kati ya fedha hizo kiasi cha Tshs.40,500,000.00 ni mkopo kutoka Halmashauri zilizokopeshwa mwezi Machi 2022 ikiwa ni asilimia 4 katika asilimia 10 zinazochangiwa katika Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu toka mapato ya ndani. Fedha hizi zilitumika kununua pikipiki 16 kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa abiria na Tsh 9,000,000.00 ni fedha zilizopatikana kutokana na shughuli za ukopeshanaji wa wanakikundi wenyewe ambazo tunaendelea kukopeshana. Aidha fedha zilizotolewa na Halmashauri zote zimerejeshwa kama ilivyotakiwa.
aidha mwenge wa uhuru umezindua mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu ya vyoo manne katika shule ya Sekondari Songwe Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha inaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia imetekeleza ilani ya uchaguzi Ibara ya 80(a) kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu manne ya vyoo yaliyojengwa katika shule ya Sekondari Songwe kwa kutumia fedha ya Serikali kuu, nguvu za wananchi
Mapato ya ndani na wadau wengine wa Maendeleo.
Mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu manne ya vyoo hadi kukamilika umetumia Tzs 114,477,200.00.
Pia kulikuwa na kongamano la vijana lengo likiwa ni kuwapa fursa vijana kujadili,Fursa za kiuchumi zilizopo wilayani Mbeya na namna ya kuzitumia,Kuwawezesha na kuwajenga vijana kuwa wazalendo na waadilifu katika Taifa, Kuwapa vijana stadi mbalimbali za maisha ili kuwafanya wawe vijana wenye kujitambua zaidi na kuchangia katika ustawi na maendeleo ya jamii, Kuwajengea vijana stadi za uongozi ili waweze kushiriki vema katika masuala mbalimbali ya uongozi katika jamii na shiriki wa vijana katika uchaguzi wa serikali za Mitaa 2024 (haki na wajibu wa kijana)
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.