Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulika na utawala Mhe George Joseph Kakunda Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Mhe Kakunda ametoa pongezi hizo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri hiyo, ambapo alitembelea kukagua miradi ya maendeleo na kisha kuongea na wafanyakazi wa Halmashauri hiyo.
Miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Mhe Kakunda katika ziara yake ni pamoja na Mradi wa Machinjio ya Kisasa ya Utengule na Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya rami Mbalizi, ambapo Naibu Waziri huyo aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kisimamia miradi hiyo vizuri.
Mradi wa Machinjio ya Kisasa ya Utengule.
Mradi huu unatekelezwa na Halmashauri kwa kushirikiana na UNIDO ambao wametoa msaada wa mashine za kisasa kwa ajili ya shughuli za uchinjaji. Akisoma taarifa ya mradi huu Kaimu Afisa Mifgo, Ndg. Kowelo amesema kuwa mradi huu mpaka sasa umetumia shilingi milioni 211 ambapo kazi zilizokamilika ni kujenga jengo la uchinjiaji, na ujenzi wa mashimo ya kuhifadhia maji taka.
Ndugu Kowelo pia amebainisha kuwa kazi ambazo bado hazijakamilika ni ufungwaji wa mashine ambazo tayari zimeshatolewa na UNIDO, ujenzi wa uzio, uingizaji wa nishati ya umeme pamoja na kujenga sehemu ya mnada wa kuuzia ngombe ambapo gharama zake zinakadiliwa kufikia shilingi Milioni 600.
Baada ya kupokea taarifa ya mradi huo, Mhe. Kakunda ameipongeza Halmashauri kwa kukamilisha sehemu ya awali ya ujenzi wa mradi huo kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha. Mhe. Kakunda amesema katika mradi huo thamani ya pesa iliyotumika na thamani ya jengo vinaendana hivyo Halmashauri inapaswa kupewa sifa yake kwa kusimamia mradi huo vizuri.
“Ni wapongeze kwa jengo lilivyojengwa hivi na sehemu zake zote zilivyojengwa mpaka sasa hivi na ubara wa flow yenyewe, kuta, mpaka ruffing kwa Milioni 211 mimi nawapongeza, naweza nikaona angalau hapa kunathamani ya fedha. Injinia na Afisa Mifugo mmemsaidia Mkurugenzi kusimamia vizuri, lakini naomba muendelee kuwa makini..”
Ama kuhusu kukamilika kwa mradi huo, Mhe. Kakunda amemuhoji Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mbeya, Ndg. Amerchioly Kulwizila anamkakati gani. Katika kujibu swali la Mhe. Kakunda, Ndg. Kulwizila amesema kuwa Halmashauri katika bajeti yake ya mwaka huu umetenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 300 toka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya kukamilisha mambo ya msingi ili machinjio hiyo ianze kutumika, lakini alisema kiuhalisia ili machinji hiyo iweze kukamilika kwa asilimia 100 shilingi milioni 600 ndizo zinazohitajika.
Baada ya kupatiwa jibu hilo Mhe. Kakunda ameigaza Halmashauri kuandaa mchanganuo wa gharama zinazohitajika kisha kuuwasilisha ofisini kwake ili aweze kuisaidia Halmashauri hiyo kupata fedha hizo kwani machinjio hiyo ikikamilika italeta tija kubwa Halmashauri na wananchi wake hivyo.
“pamoja na bajeti hii ambayo mmeiweka ya ndani, fanyeni ukokotoaji wa mahitaji yote yaliyobaki ili mradi ukamilike halafu muyalete wizarani ilituone ambavyo tunaweza kupigania, muweze kupata hii bajeti”
Mradi wa Barabara ya Rami Mbalizi
Mradi wa barabara ya rami mbalizi yenye urefu wa kilomita moja inayojengwa toka eneo la tarafani Mbalizi hadi ZKK ulianza kujengwa tarehe 27/12/2016 na ulitarajia kukamilika mwezi aprili, 2017 kwa kwa gharama ya Tsh. 613,812,654.00. lakini kutokana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo mvua kubwa zilizonyesha mwezi Aprili mwaka huu (2017) pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Serikali katika usimamizi wa ujenzi wa barabara za kwenye miji na vijijini nchini kwa kuundwa wakala anayehusika na usimamizi huo TARURA zilisababisha Mkandarasi kusimama kazi kwa muda na kupelekea muda wa mkataba kuongezeka hadi kufika tarehe 15/11/2017.
Meneja wa TARURA Mbeya Vijijini Eng. Mlelwa ambao kwa sasa ndio wanasimamia barabara hiyo amesema kuwa amesema kuwa mkandarasi ameongezewa muda huo wa mkataba bila ya kuongezeka gharama za mkataba wa awali jambo ambali limemfurahisha Mhe. Kakunda na kusema kuwa Ofisi ya Ujenzi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa ujumla zinastahili kupewa pongezi kutokana na uzalendo waliounesha katika kusimamia barabara hiyo.
Mhe. Kakunda ameseama Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imeonesha mfano wa kuigwa nchini kwa kusimamia vizuri barabara hiyo, kwani imejengwa kwa kiasi kidogo lakini kwa ubora ule ule jambo ambalo ni nadra kufanyika sehemu nyingine, hivyo ametoa wito kwa Mainjinia wengine na Halmashauri nyingine kujifunza kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
“Chapili nawapongeza kwamba mnaweza kujenga kilomita moja ya rami kwa Tsh Milioni 614 hiyo nawapongeza. Maeneo mengi unit cost ya kujenga ilomita moja ya rami yanazidi biliooni moja. Na sehemu nyingine Halmashauri moja walijenga kilomita moja la lami kwa Shilingi bilioni mbili, huo ni wizi. Nyinyi hamkufanya wizi wowote ndio maana mmebaki na kiwango kilekile cha Milioni 614, hii ni uzalendo. Na mimi natoa wito kwa wahandisi wengine, wasifikirie kwamba sisi wanansiasa na wananchi kwamba hawajaenda shule au hawajui, tunajua kila kinachotendeka. Na wakae chonjo. Ukiniwekea unit cost inayozidi 1.2 bilioni kwenye kilomita moja ya lami naanza kukuhoji…”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.