Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mwita Waitara amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa
Waitara amefanya ziara hiyo leo ijumaa julai 26,2019 kwa kutembelea mradi wa Ujenzi wa Shule ya wasichana Galijembe ambapo serikali imetoa zaidi ya shillingi Milioni 152 kufanikisha ujenzi wa shule hiyo, Kikundi cha wakinamama kinacho jishughulisha na uzalishaji wa sabuni pamoja na kikundi cha vijana kilichopewa mkopo wa pikipiki na halmashauri.
Kimsingi ziara yangu imelenga kuona ile kodi ambayo wananchi wanatoa pamoja na fedha za halmashauri na serikali kuu zinaenda kwenya miradi ya maendeleo
Waitara amesema kuwa halmashauri zinapaswa kuhakikisha kuwa asilimia 10 za makusanyo ya mapato zinatolewa kwa vijana, walemavu na wanawake kama ilivyo agizwa na serikali ilikuweza kuwainua wananchi kiuchumi, serikali ilishatoa maelekezo kuwa fedha zinazopelekwa kwa wananchi zitumike kwa malengo ya miradi husika na ndio maana leo nimepita iliniweze kukagua na kujiridhisha.
Awali akizungumza na Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya mbeya, na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Waitara amewataka watumishi kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni za Utumishi wa umma huku akiwataka watumishi kuwatembelea na kutoa huduma kwa wananchi katika maeneo yao nasi kukaa tu ofisini.
“Uhalali wa Mtumishi wa umma au kuwa eneo lolote kama mtumishi wa umma nipale ambapo atatimiza wajibu aliokabidhiwa, nasisi wasaidizi wake tumekuja hapa tukakuta umepewa mradi ukausimamie, umesimamia hovyo hovyo huwezi kubaki salama” Waitara
Pia aliwataka wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha wanatengeneza mahusiano, wanawaheshimu na kuwashirikisha wasaidizi wako katika majukomu yao na kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo katika maeneo yao kwa uweledi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.