Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia upande wa elimu.Ndg. Tixon Nzunda ameiongezea Halmashauri ya wilay ya Mbeya kiasi cha shilingi milioni 152 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya sekondari wasichana Galijembe baada ya kulidhishwa na usimamizi wa ujenzi wa miradi ya elimu.
Nzunda amesema kuwa kama ofisi yake imeamua kuongeza kiasi hicho cha pesa bada ya kuona jitiada za halmashauri na wananchi katika kutekeleza Ujenzi wa shule hiyo kwenye ziara yake ya kikazi katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
“ ofisi ya mkoa waandikieni hawa barua ya kuwapongeza kazi walioifanya ni nzuri na niwapongeze Ndugu zangu mmefanya kazi nzuri mmenifurahisha mnoo kama wizara tunachagia kiasi cha shilingi milioni 152 kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili hivyo jitaidini hizo fedha ziweze kukamilisha mambweni hayo.” Nzunda.
Shule ya sekondari wasichana Galijembe ni Ilianza kujengwa mwaka 2008 kwa nguvu za wananchi ambapo wananchi waliweza kujenga jumla ya madarasa 8 yenye thamani ya shilingi milioni 80 na baadae Wananchi kuamua kukabidhi majengo hayo kwa halmashauri ili kuweza kuendeleza Ujenzi huo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.