Wajumbe wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi wamemchagua tena Ndg Juma Makelele Kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo.kwa awamu nyingine ya mwaka wa fedha 2017/2018. Afisa Tawala Wilaya Ndg. Amimu Mwandelile amemtangaza Mhe. Juma Makelele kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi kwa kupata kura tisa dhidi ya kura saba alizozipata Ndg Diphasi Mwakisale Kwenye Mkutano wa uchaguzi wa kumchagua Makamu Mwenyekiti na kuunda kamati za kudumu za Mamlka ya Mji Mdogo Mbalizi.
Kabla ya kutangaza matokeo Ndg. Mwandelile aliwaeleza wajumbe kuwa kwa mujibu wa Sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kwamba Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mjimdogo anadumuu madarakani kwa muda wa miaka mitano lakini makamu wake anachaguliwa kila baada ya mwaka mmoja. Baada ya kusema hivyo akampa nafasi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Ndg. Juma Makelele kujiuzuru nafasi yake kabla ya kugombea tena, kisha uchauzi ukaanyika na kumtangaza Ndg. Juma Makelele ameshinda tena nafasi hiyo.
“kura zilizopigwa zilikua ni 16, hakuna kura iliyoharibika, kasoro mjumbe mmoja tu hakuudhuria, nataja kura zilizopatikana, Ndg. Diphasi Mwakisale amepata kura saba, Ndg. Juma Makelele amepata kura tisa. Kwa hiyo kwa mamlaka niliyopewa kama msimamizi wa uchaguzi namtangaza rasmi Juma Makelele kuwa Makamu Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Mbalizi”
Akitoa shukurani zake kwa wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mbalizi, Ndg. Makelele amesema kuwa sasa ni wakati wa kazi, uchaguzi ushaisha nay eye binafsi anahesabu kuwa wajumbe wote walimchagua yeye hivyo kwake hakutakuwa na tofauti yoyote. Pia aliwaomba wajumbe wasisite kumkosoa na kumshauri pale atakapokosea kwa lengo la kuijenga mamlaka hiyo.
“Ndg wajumbe nipende tu kuwashukuru kwa kazi nzuri mliyoifanya nawashukuru sana, wale walioweza kunipa kura na ambao hawajanipa nasema kwamba wote wamenipa. Nawashukuru sana naoma ushirikiano tuzidi kusonga mbele., Pale kwenye mapungufu naomba niambiwe, hakuna mtu ambaye hakusolewi wakati kunaonekana kunatatizo. Ili tufanye kazi tuimizane weto wajumbe tupo kitu kimoja, pale tunapokosea tuambizane, tusonge mbele ili mamlaka yetu isonge mbele, nawashukuru sana, asanteni sana”
Baada ya kumchagua Makamu Mwenyekiti, Mtendaji wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi, Ndg. Kassimu Ugulumo aliwatangazia wajumbe kuwa hatua inayofuata ni kuunda kamati za kudumu,ambazo ni; Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Miji. Alisema kwa mujibu wa kanuni kamati hizo zinaundwa kwa Mwenyekiti wa Mamlaka kupendekeza majina ya wajumbe na kisha majina hayo kujadiliwa na kupitishwa na Mamlaka. Hivyo kama kunamapendekezo yoyote wanapenda kuyawasilisha kanuni zinawaruhusu.
Kisha akaongeza kwamba baada ya kupitisha kila kamati itamchagua mwenyekiti wa kamati yake ambaye kwa mujibu wa kanuni ataingia moja kwa moja kwenye kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Miji wakiungana na wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao; yaani Mwenyekiti wa Mamlaka, Makamu Mwenyekiti pamoja na Mhe. Mbunge pamoja na wengine wanaopendekezwa na Mwenyekiti wa Mamlaka.
“hatua inayofuata ni kuunda kamati za kudumu, kwa kanuni zilizopo Mwenyekiti anatoa mapendekezo, lakini hayo mapendekezo yanaweza kujadiliwa lakini kama yanaafikiwa yanapita kama yalivyo, na ntakapowataja hawa waliopendekezwa watatoka nje watachaguana mwenyekiti, kila kundi litachagua mwenyekiti.wake. Wale wenyeviti ndio watakaokuwa wajumbe moja kwa moja wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Miji… mwenyekiti anamamlaka ya kuwateua wengine kuingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Fedha.”
Baada ya zoezi hilo kukamilikwa kwa amani na utulivu Mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza aliwapongeza wajumbe wote kwa hatua nzuri waliyofikia na kuwataka waongeze mshikamano katika mambo ya kimaendeleo ili kuiwezesha Mamlaka hiyo kukidhi vigezo vya kuwa Halmashauri ya Mji.
“Nianze kwa kushukuru tena kushukuru sana kwa hili zoezi la uchaguzi kuisha vizuri. Mbeya Vijijini kwa kweli kwa ujumla hasa Mbalizi nafikiri tunakwenda vizuri na nafikiri twende vizuri hivyo hivyo. Sasa naomba katika kipindi hiki kilichobaki tuwe na msimamo huo ili tuione Mbalizi yetu tuiletee mabadiliko. Katika kipindi hiki sisi ndio viongozi wa Serikali ya Mji Mdogo wa Mbalizi tukisaidiana na wataalamu wetu. Ndugu zangu tunamajukumu makubwa sana, na wananchi wanamategemeo makubwa mno, kwa hiyo naomba sana tena sana hizi kamati zilizoundwa tusione hiki kitu ni cha Diwani, Hiki kitu ni cha Mbunge hiki kitu ni cha Serikali kuu. Kwenye eneo lako uliko kitu cha maendeleo ni cha kwako”
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.