“Mafanikio haya nikwasababu ya uadilifu na usikivu mlio kuwa nao katika kipindi chote ambacho nilikuwa kiongozi wenu, ikapelekea tuwe vinara katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato pamoja na mbio za mwenge wa uhuru”amezungumza Amelchiory Kulwizila aliye kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa muda wa miaka miwili , 2016-2018.
Kulwizila ametoa kauli hiyo wakati wa makabidhiano ya ofisi na mkurugenzi mtendaji mpya Stephe E.Katemba yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri Agosti 23/ 2018.
Agosti 14, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa wakurugenzi wapya pamoja na kuwabadilisha wengine katika vituo vyao vya kazi ambapo Katemba alihamishwa kutoka Manispaa ya Kigamboni kwenda Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Aidha Kulwizila amewataka watumishi wa Halmashauri hususani wakuu wa Idara naVitengo kuendeleza kalba yao ya kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi mtendaji mpya ilikuweza kufikia dhamira na dira ya halmashauri.
Naye mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Stephen E. Katemba aliyekuwa anakabidhiwa kijiti amemwakikishia Kulwizila kuwa atahakikisha anatimiza ndoto alizo kusudia katika kuendeleza maendeleo ya Halmashauri na kuwataka watumishi wote kuhakikisha kila mmoja anaonyesha umuhimu wake katika utendaji kazi ili kila mmoja amuone yeye wamuhimu kuliko mwezake kwani kwake kukua katika utendaji kazi ni kigezo kimojawapo kitakacho mpandisha nayeye.
“ Kwangu mtu anayetaka kukua napenda akue kwani naamini wao wakikua na mimi watanipandisha kwani ndoto yangu nikuwa zaidiya hapa”Katemba.
Vitu walivyokabidhiana katika tafrija hiyo ni pamoja na orodha ya wakuu wa idara na vitengo, idadi ya madiwani,hali halisi ya ujenzi wa vituo vya afya, kesi zilizoko mahakamani pamoja na cheti cha makabidhiano.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.