Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ndugu Lodric Lazaro Mpogolo amefanya kikao leo tarehe 2 Novemba 2023 na wafanyakazi wote wa ngazi ya kata ya Nsalala, Utengule Usongwe na bonde la Usongwe wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mpogolo amefurahishwa na muitikio wa wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kuja kusikiliza na kutoa kero zao, “nimefurahi sana kuona wafanyakazi wengi kiasi hichi, nikili tu kuwa ndio mara yangu ya kwanza kukutana na wafanyakazi ngazi ya kata, na nimefurahi sana kuwaona wengi kiasi hichi” alisema Bombo
Aidha ameongeza kuwa kikubwa kilichopelekea kuitisha kikao hicho ni kukaa pamoja na wafanyakazi na kutatua changamoto walizonazo pia kushauriana namna bora ya kuendesha halmashauri yetu.
Katibu Tawala amewashukuru wafanyakazi kwa kazi nzuri wananzozifanya zinazoifanya Mbeya kuonekana moja ya mikoa mizuri inayotekeleza malengo ya Serikali vizuri na kwa ufanisi unaoonekana “Mkoa wetu unaendelea kufanya vizuri kila siku na hayo yanajidhihilisha katika martokeo mbalimbali ya mitihani, watumishi ninyi ndio injini ya Mkoa” aliongeza Mpogolo.
Aidha amemshukuru Mhe Rais kwa kazi kubwa ya maendeleo ambayo anaendelea kuifanya katika mkoa wetu kwa kujenga na kuboresha shule za Sekondari, Msingi, Zahanati na vituo vya afya, “ tumshukuru sana Rais mama yetu Mhe Dkt Samia S. Hassan kwa maendelea ambayo ameyaleta katika Mkoa wetu wa Mbeya” alisema Mpogolo.
Katibu tawala aliwatoa hofu wafanyakazi na kuwataka wawe huru kuelezea kero zao ili kuweza kutatuliwa kwa nia njema ya kujenga na kufanya kazi kwa bidi bila kumuangusha Rais wetu na Jemedari wetu, mama yetu, Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wafanyakazi walitoa maoni na changamoto zao katika idara mabalimbali ambazo Katibu Tawala alimuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya kuzipatia ufumbuziwa haraka ili zisiathili utendaji kazi wa wafanyakazi.
Aidha wafanyakazi wamefurahi sana kwa kiongozi mkubwa kuhitaji kuzungumza nao na kutatua changamoto walizonazo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.