Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Mhe. Jacobo Mwakasole amesema kuwa miradi ya maendeleo ikisimamiwa na kutekelezwa vyema, itasaidia kuondoa chuki ya wananchi dhidi ya Serikali yao.
Mhe. Mwakasole amesema kuwa chuki ya wananchi dhidi ya Serikali yao inajengwa pindi wananchi wanaposhindwa kuielewa Serikali yao haswa katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Hivyo ameziomba Halmashauri zote nchini kusimamia vyema miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwani jambo hilo litasaidia wananchi kuiamini Serikali yao na kukiamini chama kilichopo madarakani.
“Lazima Halmashauri isimamie vizuri miradi ya wananchi,, maana miradi ya wananchi isiposimamiwa vizuri, tunafanya wananchi washindwe kuielewa Serikali yao. Na kama hawata ielewa Serikali yao maana watakichukia hata chama kilichounda Serikali.”
Mhe. Mwakasole amesema hayo wakati Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mbeya ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. Kisheria Kamati ya Siasa inajukumu la kukagua utekelezaji wa Irani ya chama kilichopo madarakani kwa kufanya ziara ya kuitembelea miradi husiaka. Katika ziara hiyo kamati imefanikiwa kukagua jumla ya miradi saba ya maendeleo, ambayo ni; mradi wa kuwawezesha kiuchumi makundi ya wanawake na vijana, mradi wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF), mradi wa usambazaji umeme vijijini (REA), mradi wa maji wa Izumbwe, Iwindi, Mwahiwawala, mradi wa ujenzi wa baraba ya umalila iliyopo chini ya (TANROADS) na mradi wa ujenzi wa daraja la Idiwili.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.