Timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI imefurahishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya vitatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. Juni 6 na Juni 7 timu imefanya ukaguzi katika vituo vya afya vya Ilembo, Santilya na Ikukwa.
Kiongozi wa timu hiyo, ambaye pia ni Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ndg. Avemaria Semakafu amewashukuru wananchi kwa kujitolea nguvu zao katika ujenzi wa vituo hivyo hali inayopelekea ujenzi kwenda kwa kasi kubwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali mrefu wa kufuata vifaa vya ujenzi.
“Kwa dhati niwapongeze wananchi wote, hakika mmejitoa kikamilifu kuhakikisha vituo vya afya vinajengwa. Niwasihii msikate tamaa, muendelee na moyo huo huo wa kuinga Serikali mkono kwa vitendo. Ni kweli Serikali imeleta pesa katika miradi hii, lakini pesa peke yake isingetosha kujenga vituo hivi mpaka hatua hii mliyofikia”
Aidha Semakafu amewataka watumishi wa umma wanaosimamia miradi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za matumizi ya fedha za umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imepata ruzuku ya shilingi 1,700,000,000 toka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya vitatu, ambapo Kituo cha afya Ikukwa kimepata shilingi 800,000,000/= Santilya shilingi 500,000,000/= na Ilembo shilingi 400,000,000/= Fedha hizo zinatumika kujenga jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi, chumba cha kufulia nguo pamoja na sehemu ya kuchomea taka. Ujenzi wa vituo hivyo ulianza mwezi februari, 2018 na vinatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 27, 2018.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.