Chama cha waendesha bodaboda kanda ya kati Mbalizi wamkono meunga juhudi za serika kwa kutoa madawati 12 katika shule ya msingi mkombozi iliyoko halmashauri ya Wilya ya Mbeya.
Akitoa salamau za shukurani mara tu baada ya kupokea madawati hayo naye mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wazazi CCM Mbeya vijijini Mh.Jems Mwampondele amewashukuru waendesha bodadoba hao kwa kutoa kile wanacho kipata na kupeleka kwenye jamii.
“ninawapongeza sana kwa niaba ya jumuiya ya umoja wa wazazi natoa shukurani kwa kile mlicho kitoa naomba na mimi nitoe laki moja katika kuunga mkono juhudi zenu.” Mwampondele.
Akielezea namna ambavyo waliguswa katika kutoa madawati haya mwenyekiti wa waendesha bodaboda kanda ya kati ndg, Islael Mamba amesema kuwa wameamua kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha watoto hawakai chini.
“Mbali na kuwa tunafanya kazi katika mazingira magumu yaani jua letu mvua zetu na wengi wetu tunakipato kidogo lakini bado tumeguswa na swala hili na kuamua kuchanga na kutoa madawati 12” kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mkombozi.
Akisoma taarifa ya mwenendo wa shule naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mkombozi ndg. Lusekelo Sangalalla amesema kuwa shule ya Mkombozi ilikuwa na uhaba wa madawati 302 lakini baaada ya wadau mbalimba kushiriki kwa namna moja au nyingine mkiwemo nyie yamebaki madawati 80 tu.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.