Ubalozi wa Poland nchini Tanzania amekabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 139 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa ajili ya sekta za Afya na Elimu katika Kata ya Ilungu.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya Ilungu vyenye thamani ya Shilingi milioni 69.7. Na vifaa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Ilungu vyenye thamani ya Shilingi Milioni 70. Vifaa vya shule vilivyokabidhiwa ni pamoja na viti 146, meza 34,stuli 75,Vitanda 123,Magodoro 89, Jiko moja la kupikia,Kabati za viatandani 31, kompyuta mbili na Pasi Moja.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Kaimu Balozi wa Poland nchini. Dk. Ewelina Lubieniecka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Amelchiory Kulwizila aliyevipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Ifupa Kata ya Ilungu. .
Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Balozi, Dkt. Lubieniecka amesema vifaa hivyo vimetolewa na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali nchini Poland, zikiongozwa na taasisi ya Texpol kwa ushirikiano na Shirika la Light for Afrika ambalo Mwenyekiti wake ni Julius Zellah mkazi wa Poland na mzaliwa wa Ilungu. Pamoja na Kampuni ya Idopol ya nchini Poland inayotengeneza vifaa tiba. Taasisi hizo zimetoa msaada huo baada ya kugushwa na jitihada za wananchi wa Ilungu katika kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo ujezi wa kituo cha afya Ilungu..
“kwanza napenda kuzishukuru taasisi, kama vile, Light for Africa Foundation, SODI Foundation, na Textpole ambayo Julius ameileta hapa, na kuishukuru Idopol ambao ndio watengenezaji wa vifaa tiba ninavyovikabidhi kwenu, hakika ili ni jambo la kujivunia kwa kutoa vifaa tiba kwa wananchi wa Ilungu”
Akishukuru wakati wa kupokea Msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Amelchiory Kulwizila amesema msaada huo utaharakisha kufunguliwa kwa haraka kituo hicho cha afya, na pia ameahidi kupeleka madakatari ili huduma zianze kutolewa katika kituo hicho.
“naomba niseme ulimwengu mzima uko hapa Ifupa, watu wametoka Poland kuhakikisha kituo hiki kinafanya kazi. Sasa kazi rahisi ya Mkurugenzi ni kuwaletea madaktari, ili huduma za afya zianze mara moja”
Kituo cha Afya Ilungu kimejengwa na wananchi kwa kufanya harambee mbalimbali za kuchangishana fedha hali iliyowagusa wadau mbalimbali kuwaunga mkono, akiwemo na mfanyabiashara maarufu nchini Dkt. Reginald Mengi aliyechangia Shilingi Milioni 25 zilizotumika kukamilisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD)
Awali akitoa salamu zake kwa wananchi Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini, Mhe. Oran Njeza amewapongeza wananchi wa Ilungu kwa jitihada walizozionesha kwani zimeweza kuwagusa watu wengi wanaopenda maendeleo na kuwafanya hata watu wa Poland kufika kijiji hapo.
“Angalieni mlianza kama kamchezo, lakini leo tumekuja na ugeni huu hapa, kwa shughuli moja tu, kwa kazi moja tu mlioifanya, ya ujenzi wa kituo cha afya. Kwa kweli hii ni chachu na ninaimani mambo makubwa yatazidi kuja Ilungu”.
Naye Mganda wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Louis Chomboko amesema uwepo wa Kituo cha Afya katika Kata ya Ilungu kitawapunguzia umbali wananchi kufuata matibabu katika Hospitali teule ya Wilaya iliyopo Ifisi ambako kuna umbali wa zaidi ya Kilomita 60.
Alisema mbali na umbali huo pia miundombinu ya barabara kutoka Kata hiyo hadi kufikia Hospitali ni mibovu jambo linalohatarisha afya za wagonjwa wakati wa kusafirishwa..
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.