Baraza la madiwani halmshauri ya wilaya ya Mbeya limepitisha rasimu ya bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 47,160,060,466 kitakacho kusanywa na kutumika kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Akisoma rasimu ya bajeti hiyo mbele za baraza la madiwani, Afisa mipango wa Halmshauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Omary Haji amesema kuwa katika mwaka 2020/2021 halmashauri inakusudia kuratibu shughuli mbalimbali ikiwemo;
ununuzi wa shamba ekari 3 kwa ajili ya kuanzisha shamba la uzalishaji wa parachichi ,kuendelea kutoa elimu bila malipo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, kuendeleza ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na kuendelea kutoa mikopo na elimu ya wajasiriamali kwa wanawake, vijana na walemavu.
Katika bajeti hiyo miradi ya kipaumbele itakuwa ni ujenzi wa jengo la utawala, ununuzi wa gari, kurudisha asilimia 20% ya mapato ya ndani katika vijiji, kuwezesha ukarabati wa miundo mbinu ya kijamii, utoaji wa mikopo wa vikundi vya akina mama, vijana na walemavu.
Aidhi baadhi ya madiwani wametoa maoni kuhusu rasimu ya bajeti hiyo kwa menejimenti ya halmashaui ya wilaya ya Mbeya kuhakikisha inasimamia vyema shughuli zilizo pangwa kwa mwaka huo ilikuweza kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Afisa mipango wa Halmshauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Omary Haji Akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2020/2021 katika kikao cha baraza la bajeti
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wakiwa katika kikao cha Baraza la bajeti kwa mwaka 2020/2021
Diwani Vitimaalumu Mh Pili Adson Mwantowe, kata ya Santilya {CCM} Akichangia hoja katika kikao cha Baraza la bajeti kwa mwaka wa 2020/2021
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.