MKUU wa Wilaya ya Mbeya ,William Ntinika ameagiza halmashauri ya wilaya ya Mbeya kubuni vyanzo vya mapato vya ndani ili iwe na uwezo wa kujitegemea yenyewe.
Ntinika amesema hayo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri cha wilaya(DCC) kilichokuwa kikijadili Rasimu ya bajeti ya halmasahauri ya Wilaya ya Mbeya kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambacho kiliwashirikisha viongozi mbalimbali wa Wilaya .
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa halmshauri kama wana ardhi nzuri kwanini wasifanye ubunifu wa kujenga shule ambayo itakuwa chanzo cha mapato ya ndani .
“Wenzenu Halmashauri ya Jiji wana wana shule tatu ambazo ni Magufuli,Azimio , Mkapa hizi zote zinawaingizia mapato ya ndani na sasa wana shule inajengwa itaitwa Nsalaga na tayari Mkuu wa Mkoa na timu yake walikuwa huko kukagua muda si mrefu itakamilika ,na nyinyi kama halmashauri ya wilaya na mna ardhi nzuri kwanini msifanye ubunifu huo mkajenga na watu wapo tayari hivyo ni vyanzo vya ndani ili halmashauri iwe na uwezo wake wa kujitegemea”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo Ntinika alisema kuwa kati ya fedha Bil.56 mapato ya ndani ni Bil.4 kwa maana ina uwezo wa asimilia 8 na kuwa asimilia 82 inategemea kutoka serikali kuu na kwamba mwaka jana waliletewa bil.1 .7 ambazo zimejenga vituo vya afya vya Santilya .mil.500,Ikukwa,mil.800,Ilembo,mil.400 na ndo sababu Rais alisema halmashauri ianze kujenga vituo vya afya .
Aidha Ntinika alitoa wito kwa halmashauri kupitia wataalam wake kuendelea kuwa wabunifu jinsi ya kuwa na vyanzo vya mapato ya ndani ambavyo vitasaidia ili halmashauri iweze kujitegemea .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa wazazi wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Mbeya(CCM) ,William Simwali alisema halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imekuwa ya mfano kwa kutoa mafuta kinga na vifaa saidizi kwa watu wenye ulbino.
Simwali alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ni halmashauri pekee kwa Mkoa wa Mbeya ambayo imekuwa mkombozi kwa kutoa fedha zake za mapato ya ndani kununua mafuta kinga kwa watu kwa wenye ulbino,Mbeya , Songwe,Rukwa kwa kutenga fedha kutoka mapato ya ndani kununua mafuta kwa ajili ya watu wenye ualubino.
Aidha alishauri serikali kuhakikisha kuwa kila halmashauri inatenga fungu maalum kwa ajili ya kupata mafuta kinga na vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu kwani watu wenye ulbino adui wao mkubwa ni salatani ya ngozi ambayo inawafanya washidwe kufikisha hata miaka 40 .
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.