Jamii kwa kushirikiana na ustawi wa jamii wametakiwa kuwabaini watoto wote wanaokinzana na sheria na kuwapeleka katika kituo cha maadilisho ili kuweza kupunguza waarifu katika maeneo yetu.
Hayo yamebainishwa na Afisa Tawala wa Wilaya ya Mbeya ndug. Amimu Mwandelile wakati wa zoezi la kupeleka zawadi za sikukuu za Eid El Fitril zilizo tolewa na Mh. Rais katika kituo cha kulelea watoto walio kinzana na sheria cha shule ya msingi Maadilisho Ilambo kwa lengo la kuwafanya watoto hao kuona serikali na jamii ipo pamoja nao.
Naye meneja wa kituo cha Maadilisho Ilambo ndug. Mustafa Mjema amefafanua kuwa kituo hicho kinachukua watoto walio kinzana na sheria kutoka pande zote za Tanzania.
Mjemba ametaja makosa yanayosababisha watoto kukinzanaa na sheria kuwa ni pamoja na ubakaji, ulawiti, wizi, pamoja na kustisha masomo.
“Wazazi wengi wanakuwa na wasiwasi wa kuwapeleka watoto wao katika vituo wakiona kama ni sehemu ya magereza lakini niwatoe hofu kwani katika eneo hili tunawafundisha watoto mambo mengi sana ikiwemo jinsi ya kuishi na jamii, na wakirudi huko jamii iachane na tabia ya kuona wao ndio chanzo cha maovu wakiwa wametoka huku”
Kituo cha maadilisho kinachukua watoto kutoka pande zote za Tanzania kwa sasa kinawatoto wapatao 25 wa umri kuazia miaka 12 mpaka 17 kituo hicho kipo Wilayani Mbeya Kata ya Igoma kijiji cha Ilambo kilichopo chini ya Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.