Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imeendelea kutekeleza ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya shule za Sekondari ambazo zimepatiwa fedha kutoka Serikali Kuu na SEQUIP. Kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, ofisi, vyoo na maabara.
Shule zilizopatiwa fedha hizo ni pamoja na Songwe ambapo wamepatiwa milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa, vyoo na ofisi moja ya walimu. Shule ya Sekondari Songwe ipo katika kata ya Bonde la Usongwe katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Shule ya Sekondari Songwe inatarajia kuanzisha kidato cha tano ifikapo Julai 2024 ambapo itapokea wanafunzi wa kwanza wa kidato cha tano shuleni hapo.
Aidha shule ya Isuto yenye kidato cha kwanza adi cha nne pia imepatiwa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu. Madarasa hayo yatatumiwa na kidato cha tano wanaoanza Julai 2024.
Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imepatiwa fedha za kuendeleza kujenga madarasa mengine mawili katika shule mpya ya Sekondari Iyawaya inayojengwa kwa fedha za SEQUIP wameongeza madarasa mawili ili kutumika kwa wanafunzi watakao chaguliwa kujiunga na shule hii kidato cha kwanza. Shule ya Sekondari Iyawaya hadi sasa inawanafunzi wa kidato cha pili na chakwanza watakaoanza mwezi wa kwanza.
Pia MbeyaDC wamepatiwa fedha za SEQUIP milioni 55 kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa katika shule ya Sekondari Iyelanyala ambapo wanategemea kupokea wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na shule hii.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.