Wakuu wa idara na vitengo sita kutoka halmashauri za mkoa wa Mbeya wameanza kupatiwa mafunzo rasmi ya mfumo mpya wa manunuzi ya serikali unaofahamika kwa jina la National Procurement System of Tanzania ( NEST).
Halmashauri hizo ni Mbeya Jiji, Mbeya DC, Rungwe, Kyela, Mbarali, na Chunya ambapo wakuu wa idara na vitengo wanaopatiwa mafunzo hayo ni Afisa manunuzi, Afisa mipango, Afisa TEHAMA, Afisa Habari, Afisa Ukaguzi na Mwanasheria.
Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya na yanatarajiwa kudumu kwa muda wa siku tano kuanzia leo Agosti 23 - 27/2023huku yakitarajiwa kuwa na manufaa makubwa katika manunuzi katika halmashauri hizo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.