Wafanyabiashara wa Stationery katika halmashauri ya wilaya Mbeya wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa TAUSI kwaajili ya kuomba leseni ya biashara zao pamoja na kuwasaidia wafanyabiashara wengine pindi wanapohitaji kuomba leseni hizo.
Akiongea mara baada ya mafunzo hayo Afisa Biashara halmashauri ya wilaya mbeya Elizabert Lyombe amesema lengo la kuwapatia mafunzo hayo ni kuondoa kero inayowapata wafanyabiashara pindi wanapohitaji kuomba leseni ya biashara ambapo hapo awali wafanyabiashara walikuwa wakilazimika kwetembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma hiyo.
Lyombe amesema kwasasa wafanyabiashara wanaweza kupata huduma hiyo kwenye stationary zilizokaribu yao, hivyo wameweza kuokoa usumbufu wa muda pamoja na kutembea umbali mrefu kwaajili ya kupata huduma hiyo.
Kwa upande wao wafanyabiashara hao wameishukuru serikali kwakuwapatia mafunzo hayo kwani yatawasaidia kupanua wigo wa biashara zao pamoja na kutatua kero ya kuomba leseni za biashara zao kwao na kwa wafanyabiashara wengine
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.