Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ally ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa kusimamia miradi ya maendeleo na kutekeleza maagizo ya serikali kwa uweledi, ufanisi na uadilifu.
Mkonge aliyasema hayo wakati wa makabidhiano ya mwenge wa Uhuru kati ya halmashauri ya wilaya ya Mbeya na halmashauri ya wilaya ya Busokelo yaliyo fanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Lugombo.
“Nikupongeze sana Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwani ile asilimia 10 inatolewa kwa wahusika ipasavyo nijambo jema sana,niwapongeze tena viongozi wote wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa miradi mizuri ya maendeleo kwani mnafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu.” Mkongea
Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya wilaya ya mbeya umepitia miraddi mbalimbali ikiwemo kukagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,Ufugaji wa Samaki, Kuona mradi wa Uhifadhi wa chanzo cha Maji, shule ya wasichana Galijembe na Utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu.
KWa habari zaidi Bofya link hapa chini
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.