Wakulima wa Kata ya Inyala Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wametakiwa kujihadhari na wadudu waharibifu wa mazao aina ya viwavijeshi kwa kusafisha mashamba kutokana na kuwepo kwa viashiria vya wadudu hao kwa nyanda za juu kusini.
Wito huo umetolewa na Afisa kilimo mkuu kutoka wizara ya kilimo, Ndg Jubilant Mwangi wakati wa mafunzo kwa wakulima ya jinsi ya kujikinga na wadudu hao yaliofanyika kata ya Inyala mkoani Mbeya.
Mwangi alisema kuwa Serikali imejipanga kutoa elimu kwa wadau na wakulima juu ya kutambua namna ya kuwathibiti,kusambaza mitego ya kutabiri uwepo wa viwavi jeshi vamizi,pamoja na kutoa viwatilifu vya kupambana na wadudu.
Aidha kwa upande wa nyanda za juu kusini jumla ya mitego 100 itasambazwa kwaajili ya kuthibiti na kutabiri uwepo wa viwavi jeshi vamizi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.