Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ndg, Stephen E. Katemba amegawa na kuwasainisha waleze wa kata na watendaji wa kata mikatamba ya makubaliano ya utekelezaji wa ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Zoezi la usainishajiwa wa mikataba limefanyika katika ukumbi wa halmashauri kwenye kikao cha mkurugenzi, wakuu wa idara na vitengo pamoja na watendaji wa kata chenye lengo la kuwafahamisha watumishi hao majukumu yao katika zoezi hilo.
Katemba amesema kuwa kila mtu anatakiwa kujua kuwa anawajibu mkubwa wa kutekeleza agizo la mweshimiwa rais,hivyo mbali na kuwa na majukumu yao ya kila siku suala la ugawaji wa vitambulisho lipewe kipaumbele.
“ugonjwa utatoka wapi na kipindi hiki cha ugawaji wa vitambulisho kama kuna mtu anashidwa kufanya kazi et kwa kisingizio cha kuumwa atupishe tutafute wengine , kila mtu anaishi na kula anacho tafuta lazima apewe kitambulisho, iwe mkulima, mfugaji, mpiga debe, mbeba mizigo na wengine wote.”Katemba
Halmashauri ya wilaya ya mbeya imepewa jumla ya vitambulisho 5000 kwa awanu ya pili huku kwa awamu ya kwanza ilipewa vitambulisho 900 ambavyo mpaka sasa vyoye vimesha gawiwa kwa wafanyabiashara wadogo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.