Walimu wa shule za msingi na sekondari kuanza kupimwa utendaji kazi wao kwa kuzingatia ongezeko la kiwago cha ufaulu wa wanafunzi wanao wafundisha.
Hayo yamezungumzwa na Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)anayeshughulikia upande wa elimu.Ndg. Tixon Nzunda wakati wa ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Nzunda amesema kuwa kwa zama hizi kila mwalimu atapanda cheo kwa kutazama utendaji kazi wake wa kila siku kwa kuangalia mifumo ya ufundishaji darasani.
“kila mwalimu ahakikishe anafanya kazi kwa bidii na ubunifu na kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kuhakikisha anaandaa mifumo ya kufundishia darasani kama vile andalio la somo, mpango kazi,pamoja na kuhakikisha vipindi vyote vinafundishwa kama vilivyo pangwa kwa muda husika ”. Alisema Nzunda
Ziara ya naibu katibu mkuu wa TAMISEMI- ELIMU ilikuwa na lengo la kubaini matumizi ya fedha za serikali zinazopelekwa mashuleni kama zinafanya kazi husika ,ufaulu wa watoto pamoja na jinsi viongozi wa ngazi za mikoa na serikali za mitaa wanavyo simamia majukumu yao kwa upande wa elimu.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.