Kamati ya Fedha, Uongozi na Utawala imewashauri watalamu wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kuhakikisha inakagua, kutembelea pamoja na kushauri kitaalamu miradi inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi iliiendane na ubora uliopangwa na serikali.
Kamati ilitoa ushauri huo wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha robo ya tatu.
Mbali na ushauri huo pia kamati imewashauri wananchi wa maeneo mbalimbali kuendelea kuchagia katika miradi ya maendeleo pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali na si kuiachia serikali peke yake.
“Viongozi mna kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanashiriki katika katika ujenzi wa miradi ya maendeleo, kwani wenye uhitaji ni sisi hatutegemei kuona nyie mpo nyuma katika kutekeleza miradi hii. Kila mmoja ana wajibu wa kuchagia na kuona miradi inakamilika kwa wakati na kusimamia matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali.” Makamu mwenyekiti wa halmshauri Mh. Ezekia Soda Shitindi.
Katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya tatu kamati ya fedha, Uongozi na Utawala ilifanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari Juhudi na Songwe kuona ununuzi wa madawati , kutembelea ukarabati wa bweni na ununuzi wa vitanda katika shule ya sekondari Iwindi, ujenzi vya vyoo katika shule ya Malama sekondari, kutembelea shule ya msingi Kawetere, zahanati ya Idimi pamoja na ujenzi wa njia za kuunganisha majengo na kichomea taka katika hospitali ya wilaya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.