Wakazi wa kitongoji cha Itete kilichopo katika kijiji cha Iwanza kata ya Ihango halmashauri ya wilay ya Mbeya wametakiwakushirikiana na serikali katika ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kuboresha miundombinu iliyoko katika kijiji hicho.
wito huo umetolewa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg Gidion Mapunda wakati wa ziara ya kutembelea kitongoji hicho kwa lengo la kujua maisha wanayo ishi wananchi hao ilikuweza kubaini changamoto wanazo kumbana nazo.
Mapunda amesema kuwa kila mwananchi ajione kuwa anajukumu la kuhakikisha ujenzi wa madarasa katika kituo hicho unakamilika kwa wakati ilikuweza kunusuli hali iliyopo kwa sasa ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule iliko.
Mbali na hayo mapunda ameutaka uongozi wa kitongoji cha Itete kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya kitongoji hicho ilikutoa sitofahamu kwa wananchi wanao changia mapato hayo na kuendeleza dhana ya ukweli na uwazi pamoja na kutoa risiti kwa wananchi wote wanao toa michango husika.
katika ziara hiyo ya wakuu wa idara na vitengo halmashauri ya wilaya ya Mbeya walifanikiwa kutembelea pia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kituo shikizi cha Ipinda,Iwanza pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Utengule Usongwe.
Wananchi wa Itete ni jamii iliyojitenga na jamii nyingine ambayo inaishi umbali wa kilomita tano(5) kushuka chini kutoka kilipo kijiji cha Iwanza. Katika kitongoji hicho kunawanafunzi wanao kadiliwa kuwa ni 280 kuanzia awali mpaka la saba ambao baadhi yao hudumaza masomo wanazipata katika shule ya msingi Mbeya Peak.
Wakuu wa Idara halmashauri ya wilaya ya Mbeya wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ndg Gidion Mapumba wakizungumza na wakazi wa kitongoji cha Itete kata ya Ihango .
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.