TANAPA yapongeza Wananchi wa kijiji cha Ifupa kata ya Ilungu tarafa ya Tembela Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa ushirikiano walioutoa wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa nyumba ya mganga wa zahanati ya Ifupa.
Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa hifadhi ya TAIFA YA kitulo ACC Teodora A. Batiho alipokutana na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya halmashauri ya wilaya ya mbeya wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa wa 2019/2020 .
Akizungumza na Kamati Teodora amesema anaupongeza uongozi wa kijiji pamoja na wananchi kwa ushirikiano walioutoa wa kuchangia nguvu kazi katika utekelezaji wa mradi huo.
“Kijiji hiki kwa kweli kimekuwa ni cha mfano tumetekeleza miradi kama hii sehemu nyingi ila hawakuweza kuwa na ushirikiano kama ulivyo hapa, kijiji hiki kimetoa ushirikiano mzuri na wakutosha ndio maana tumeweza kukamilisha mradi huo kwa wakati”,Teodora.
Kwa niaba ya kamati hiyo naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mh. Kisemba Mwalingo ametoa pongezi kwa Uongozi wa TANAPA kupitia hifadhi ya Kitulo kwa ufadhili wa ujenzi wa nyumba ya Mganga
“Niwapongeze kwa kazi mnazozifanya TANAPA za kuhifadhi rasilimali zetu ambazo pia zinatuleta mapato na sisi tumeona mfano wa nyumba hii ni mapato yanayotokana na kazi ya uhifadhi wa rasilimali mnazofanya”. MWALINGO.
Hifadhi ya kitulo kupitia idara ya ujirani mwema inatekeleza Ujenzi wa nyumba ya mganga wa zahanati ya Ifupa yenye thamani ya shilingi milioni 86 huku TANAPA wakiwa wamechania nilioni 67 na wananchi milioni 19 mpaka mradi ukamilike ambao kwa sasa ujenzi upo katika hatua za mwisho.
Hata hivyo kamati ilipata fursa ya kutembelea miradi mingine kama shule ya sekondari Galijembe, shule ya sekondari Utengule Usongwe, ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Izumbwe II, Kutembelea daraja la Isende, ukaguzi wa ujenzi wa soko la Tunduma Road, pamoja na Kutembelea Zahanati ya Idimi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.