Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso amekemea vikali tabia ya wananchi wa kijiji cha Nsenga,kata ya Swaya ya kuharibu miundo mbinu ya maji kwani serikali imekusudia kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani.
Karipio hilo amelitoa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maji Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya septemba 24,2018 akiwa anapokea taarifa kutoka kwa diwani wa kata ya Swaya Mhe. Julius Ntokani yakuwa wananchi wa Nsenga wamekuwa na tabia ya kuhujumu miundo mbinu ya maji ikiwemo kukata mabomba mara kwa mara hata yakifanyiwa marekebisho.
Aweso amesema kuwa serikali inafahamu kuwa wananchi wanahitaji maji safi na salama hivyo imekusudia kutoa na kusimamia huduma bora za maji kama wananchi wanatakiwa kuacha tabia hiyo mara moja.
Kwa upande mwingine naye Mbunge wa jimbo la Mbeya vijiji Oran Njeza amemuomba waziri wa maji na Umwagiliaji kuwaangalia kwa ukaribu na kwa huruma wananchi wa jimbo la Mbeya vijiji kwani wanauhitaji mkubwa wa maji safi na salama.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.