Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila ameushauri uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kuweka utaratibu wa kukopesha daladala, matipa, matrekta na pawatila kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu wale wanaorudisha mikopo kwa wakati ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Chalamila ametoa ushauri huo wakati wa zoezi la utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu liliofanyika katika uwanja wa Miyombo uliopo kata ya Inyala.
“halmashauri ya wilaya ya Mbeya ni halmashauri ya kwamza kimkoa inayoendana na kasi ya serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo, mkurugenzi na mkuu wa wilaya kwa sasa anzeni kuwakopesha hao vijana matipa na daladala ili vikundi vilivyofuzu vizuri vianze kuhama kutoka kwenye kukopa bodaboda kwenda kwenye kosta na kutoka kwenye kosta kwenda kwenye matipa na wale wanaojishughulisha na shughuli za kilimo wakopeshwe matrekta.
Akisoma taarifa ya mwenendo wa mikopo katika halmashauri naye afisa maendeleo wa halmashauri Bi zena Kapama amesema kuwa katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2019/2020 (aprili mpaka juni) halmashauri imetoa kiasi cha shilingi million 243 kwa vikundi 16 vya wanawake, vijana na walemavu.
Nao wanufaika wa mikopo hiyo wameahidi kutumia vizuri mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia katika kusomesha watoto na kutatua matatizo madogo madogo katika jamii na si kutumia vibaya.
“mikopo hii nitaitumia vizuri kama unavyoona haina riba hivyo nitahakikisha natumia vizuri kwani itatusaidia kusomesha watoto hivyo nawashauri wenzangu kuacha kabisa kutumia pesa vibaya ikiwa ni pamoja na kuhonga na kulewea pombe.” Nuru Sanga.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.