Wanawake wajasiriamali Mkoa wa Mbeya wametakiwa kuhakikisha wanarasimisha biashara zao
ilikuweza kujiongezea uhuru katika kufanya kazi zao.
hayo yamebainiwa na Mgeni rasmi afisa biashara wa halmshauri ya wilaya ya Mbeya Bi. Elizabeth
Lyombe wakati wa Kilele cha mafunzo kwa Wajasiriamali Wanawake ya Financial Literacy for Women
Entrepreneurs yaliyofanyika kakita Ukumbi wa Tughimbe jijini Mbeya.
Bi Elizabeth amewapongeza wanawake na waratibu wa mafunzo hayo na kuwahasa
wajasiriamali wanawake kuhakikisha wana rasimisha biashara zao na kuhakikisha wanakuwa na
vitambulisho vya wajasiriamali.
Akijibu kero za Washiriki wa mafunzo hayo bi Elizabeth amesema swala la kukosa mtaji kwa
wajasiriamali Wanawake kwa sasa serikali imeliona hilo na kwenye Halmashauri zetu kupitia
mapato ya ndani kunamiongozo ambayo inatuongoza kutoa mikopo kwa wanawake
“Tuna asilimia 4 za Wanawake asilimia 4 za vijana na asilimia 2 kwa walemavu kwenye hizo
asilimia 4 za mapato ya ndani zinatakiwa zitoke tuwagawie wanawake wajasiriamali wadogo”
mikopo hiyo huwa inatolewa katika vikundi hivyo nawaomba mjiunge kwenye vikundi
ilimuombe mikopo hiyo”Bi Elizabeth
Mafunzo yaliyotolewa na Mandela Washington Fellowship yalishirikisha jumla ya washiriki
151 na kupate elimu juu ya namna ya kutunza fedha kwa kipindi cha wiki 16 lengo ikiwa ni
kuwapa elimu na Kuwajengea Uwezo Wanawake wajasiriamali juu ya elimu ya fedha katika
biashara, Umuhimu wa kutunza kumbukumbu za fedha,kutenganisha fedha ya biashara na fedha za matumizi ya kawaida pamoja na Umuhimu wa kupanga bajeti na namna ya kutengeneza bajeti.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.