Wasichana 31,396 mkoani Mbeya wenye umri wa miaka 14 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi.
Taarifa hiyo imetolewa na msaidizi wa Katibu Tawala Mkoa anayehusika na Serikali za Mitaa ndgu. Costatino Mushi katika mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya18 Aprili 2018.
Mushi amebainisha kuwa wasichana watakaopatiwa chanjo hiyo wengi wao wanapatikana mashuleni na baadhi wapo majumbani, hivyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma za chanjo ikiwemo vituo vya afya, mashuleni na baadhi ya maeneo katika jamii yaliyopagwa kutumika kwa huduma ya chanjo.
Aidha Mushi amezitaja sababu zinazo sababisha saratani hiyo kuwa ni pamoja na kufanya ngono katika umri mdogo, kubeba mimba katika umri mdogo, kujamiiana na wapenzi zaidi ya mmoja pamoja na uvutaji wa sigara.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika amewataka wajumbe hao kuhakiksha wanawaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hiyo na kuhamasisha wajitokeze kwa wingi ilikuweza kuinusuru jamii ya kizazi kijacho
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.