Waheshimiwa madiwani halmashauri ya wilaya ya Mbeya wafurahishwa na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na timu ya wataalamu wa halmashauri.
Furaha hiyo imeoneshwa wakati wa ziara ya madiwani ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2015 hadi 2020.
“ Wataalamu hawa wametusafisha, kwa muda mfupi tu wametekeleza miradi mingi, kwa kweli huko tunakorudi tuna vitu vya kuwaambia wananchi" .Mh. Esther Mbaga diwani wa kata ya Mshewe.
“ Hata kama tukirudi katika maeneo yetu kwa wananchi waliotutuma kuwawakilisha tunacho cha kusema ikiwemo kujivunia ujenzi wa vituo vya afya vya Ilembo, Santilya na Ikukwa, hospitail ya wilaya, Shule ya wasichana Galijembe, soko la tunduma Road, ujenzi wa madarasa na vyoo pamoja na stendi ya Mbalizi” kaimu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Julius Ntokani.
Katika ziara hiyo, madiwani walifanikiwa kutembelea kituo cha afya cha Ikukwa, Ilembo na Santilya ujenzi wa stendi ya Mbalizi pamoja na soko la Tunduma Road.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.