Watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauhri ya wilaya ya Mbeya wameonywa kuacha tabia ya ubadhirifu wa fedha za mapato zinazokusanywa kwenye maeneo yao.
Onyo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Ndug, Stephen E. Katemba wakati wa kikao kazi na watendaji hao chenye lengo la kuonyesha mikakati na mwelekeo wa Halmashauri kwa sasa.
Katemba amesema kuwa kama watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri makusanyo ya mapato na kuacha tabia ya kuona hela hizo ni zao, na kwa wale ambao waliweka fedha kwenye mifuko yao wajiandae kurudisha mara moja kabla ya mkono wa serikali haujaaza kufanya kazi yake.
“ Joto nililonalo kwa sasa si la kawaida najiuliza kwanini ukae na hela ya serikali mtu anamilioni tano, mbili au tatu jumla ya hela mlizo nazo ni zaidi ya milioni mia mbili sitaweza kuvumilia hili.”Katemba
Pia mkurugenzi amewataka watendaji hao kuvibaini vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye kata zao kwani huko ndo yanakotoka mapato ikiwemo ushuru wa burudani na michezo,vibali vya ujenzi pamoja na kutambua maeneo ya madini.
Aidha amemtaka afisa utumishi kuhakikisha anasimamia zoezi la kusainiana mikataba ya kazi na watendaji ilikuweza kuwabana wale wote ambao hawatatekeleza majukumu yao kikamilifu.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.