Watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri ya wilaya ya mbeya wametakiwa kuhakisha wanakuwa na tabia ya kujisomea mambo ya matumizi ya mashine za kukusanyia mapato(poss) kwajili ya kuongeza ujuzi na uelewa wa namna ya kutua mashine hiyo ilikuondokana na hali ya kukosekosea mara kwa mara.
mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya yaliyoendeshwa na wataalamu Halmashauri yenye lengo lakuwaelekeza watendaji hao namna ya kutumia mashine za kukusanyia mapato(POSS) katika kukusanyia mapato.
Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya mbeya Ndg Mpakani Kalinga amesema kuwa kama watendaji wanakazi yakuhakisha wanaongeza jitihada za kujifunza na kuongeza uelewa wa namna ya mashine za kukusanyia mapato zinavyo fanya kazi ilikuweza kuondokana na tatizo la kuwepo kwa makosa ya matumizi.
"iliufanikiwe kwenye poss ni lazima kuhakikisha kilasiku una kuwa na taarifa ya makusanyo kwa kila siku pili ni k kuhakikisha miamala yote ambayo imekosewa inatolewa taarifa mapema ili kuweza kutatua changamoto hiyo" kalinga
Naye afisa Tehama wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Benedict Millinga aliweza kuwafundisha namna ya kutoa riporti,pamoja na kuandaa taarifa kwaajili ya kupeleka na umhimu wa kupeleka pesa hizo kwa wakati.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.