Watumishi 138 kati ya 152 wamepokelewa katika halmashaurji ya wilaya Mbeya na kutakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuwapatia huduma bora wananchi katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mbeya Ndug: Stephen E. Katemba amesema katika utumishi wa umma ni muhimu kulinda rasirimali za umma na miongoni mwa rasirimali hizo ni pamoja na muda waliopangiwa katika kutekeleza majukumu kazi zao.
Mkurugenzi amewataka watumishi hao kuutumia vizuri muda wa kazi waliopangiwa, huku akiwataka kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia nafasi hizo za ajira.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya Utumishi na Usimamizi wa rasirimali Watu Halmashauri ya Wilaya Mbeya Ndugu.Nicodemus Tindwa amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwapangia watumishi 152 wa idara ya afya, elimu awali msingi na sekondari kwani halimashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa watumishi hivyo ujio wa watumishi hao kutaletasaidi kuongeza tija katika kazi.
Mwisho.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.