Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh.William Paul Ntinika amewataka wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kuhakikisha wanakamilisha mapema taratibu za awali za ujenzi wa hospital ya wilaya ikiwa ni pamoja na upimaji wa eneo hilo.
Ntinika ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kuona eneo litakalo jegwa hospital ya wilaya lililopo kata ya Inyala.
Pamoja na hayo mkuu wa wilaya amewataka wataalamu kutokukaa ofisini na badala yake wahamie eneo la ujenzi kuhakikisha wanakamilisha michoro pamoja na hatimiliki ya eneo hilo.
“Na mimi narudisha Ofisi hapa kwa sababu ndio hospitali ya kwanza ya wilaya tangu tumepata uhuru, Kero zote sasa hivi nitakuwa nasikiliza hapa Inyala.” Ntinika
Hatua za ujenzi wa hospital ya wilaya umeaza mara tu baada ya kupokea kiasi cha shilingi milioni mia tano(500,000,000/=) kutoka serikali kuu ya mpago wa kuboresha huduma ya mama na mtoto.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.