Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E. Katemba amewataka watumishi wa halmashauri kufanyakazi kwa bidii pamoja na kuwa na kauli nzuri kwa wananchi.
Katemba ameyasema hayo wakati wa kikao na watumishi wote wa makao makuu cha kujadili na kusikiliza kero mbalimbali za watumishi zinazo kwamisha utendaji kazi.
“ kuna baadhi ya watumishi wanafanya kazi kwa kujituma kiasi kwamba hata mimi mwenyewe najisikia raha kwa mfano kuna mtumishi wa idara ya maji Ndg. Wando Mwangwale na mtumishi wa idara ya ujenzi ndg. Arthur Mwakajila kwa kipindi hiki wamefanyakazi nzuri kuna muda wamediriki hata kuishi nje ya makazi yao ilikuweza kukamilisha kazi zao hivyo kila mtu nitampa kiasi cha shilingi laki tano(500,000) kama motisha” Katemba.
Pia ameitaka idara ya utumishi kuona namna ya kutafuata muundo mzuri wa kuwatambua wafanyakazi bora na kuachana na tabia ya kuchagua watumishi wasio na sifa.
Kikao hiki ni moja ya vikao vilivyo pagwa na halmashauri vinavyo kaliwa kila baada ya miezi mitatu vya kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo ya halmashauri na namna ya kuhudumia wananchi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.