Watumishi wa umma Mkoani Mbeya wameaswa kuacha tabia ya kujihusisha na ushabiki wa kisiasa na badala yake wanatakiwa kuwatumikia wananchi na kuishauri serikali kama mwongozo wa utumishi wa umma unavyowataka
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamiwa wakati wa kikao na watumishi wa umma kutoka taasisi zote zilizopo mkoani humo kilichofanyika Agosti 7,2018 kwenye ukumbi wa mkapa mjini Mbeya.
“Nawaomba watumishi wangu achaneni na mambo ya siasa kama unataka siasa chagua moja ,kazi ama siasa,kwani huwezi kutumikia mabwana wawili, fuateni mwongozo wa majukumu yenu .”Chalamila.
Mbali na hilo pia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumishi wa umma kuwatumikia wananchi ipasavyo ili kuondokana na manung’uniko kwakuwa kumekuwa na malalamiko ya wananchi ya kunyanyaswa katika ofisi za umma na utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi.
Taasisi zilizo hudhuria katika kikao hicho ni pamoja na taasisi ya Dawa na Chakula(TFDA),Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na jiji, Mamlaka ya Mapato,(TRA), Mamlaka ya barabara(TANROAD) pamoja na Mamlaka ya Marabara za vijiji na Mjini(TARURA).
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.