Watumishi Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wametakiwa kutafsiri dhana ya uhuru kwa kufanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya vituo vya afya na shule.
Hayo yamebainiwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ndug. Stephen E.Katemba wakati wa kikao na watumishi cha kuonyesha namna Halmashauri itakavyo adhimisha siku ya uhuru.
Pia katemba amewakumbusha watumishi maana zima ya uhuru kuwa uhuru wa kweli ni uhuru wa kufanya kazi kila mmoja anatakiwa kujitegemea kwa kufanya kazi hivyo sisi tutafanya kazi kwa kuokoa hela ya serikali ili iweze kufanya kazi katika maeneo mengine.
“kama halmashauri tumejipanga kufanya shughuli za kimaendeleo za kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira katika vituo vya afya vya Ilembo, Santilya pamoja na shule ya sekondari ya wasichana Galijembe.” Katemba.
Mnamo tarehe 20,Nov,2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.john Joseph Magufuli alifanya mabadiliko ya maadhimisho ya siku ya Uhuru kwa mwaka 2018 badala yake kila mkoa na wilaya wapange shughuli za kufanya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.