Kamati ya fedha na mipango robo ya pili mwaka wa fedha 2023/2024 ya halmashauri ya Wilaya ya Mbeyaimeanza ziara ya siku nne leo tarehe 16. 01. 2024 ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Elimu Msingi, Sekondari na Afya.
Ziara ya kamati ya fedha na mipango chini ya Mwenyekiti wake Mhe Mwalingo Kisemba imetembelea shule ya sekondari Iyelanyala iliopo kata ya itewe, shule ya sekondari Imezu na Iyawaya zilizopo kata ya Inyala.
Kamati ikiwa katika shule ya sekondari Iyelanyala imekagua madarasa mawili na maabala moja ya kemia ambapo zilianza kujengwa kwa nguvu ya wananchi na kumaliziwa na serikali ya awamu ya sita inayooongozwa na Rais Dkt Samia S. Hassan ikiwa ni katika kutekeleza ilani ya vchama cha mapinduzi CCM.
Milioni 55 zilitolewa na serikali kuu kwa ajili ya umaliziaji wa madarasa hayo na maabala moja ya kemia. Kamati imeridhishwa na umaliziaji wa majengo hayo ambayo tayari swanafunzi wa kidato cha nne wameanza kuyatumia mwaka huu.
Aidha kamati imepongeza juhudu za wananchi na kamati ya shule kwa usimamizi mzuri na kwendana na kasi ya awamu ya sita.
Kamati pia ilitembelea kata ya Inyala na kujionea umaliziaji wa madarasa manne na vyoo matundu mawili shule ya sekondari Imezu ambayo ilipewa milioni 96 kwa ajili ya ujenzi huo, kamati pia ilitembelea shule Jirani ya sekondari Iyawaya na kujiridhisha na ujenzi wa vyumba viwili ya madarasa.
Iyawaya ni miongoni mwa shule nyingi zilizoanzishwa na ilikuwa na kidato cha kwanza na cha pili, ongezeko la wanafunzi ndilo liliopelekea Mhe Rais kuongeza madarasa hayo mawili yenye thamani ya shilingi milioni 25 ili wanafunzi wapate sehemu nzuri ya kujifunzi. Shule ya Iyawaya hadi sasa imepokea wanafunzi 105 kidato cha kwanza.
Kamati hii ni muunganiko wa waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri.
Ahsante serikali ya awamu ya sita kwa miradi mikubwa ya maendeleo ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.