Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiongozwa na mwenyekiti wake Mhe Denis Londo Mbunge wa Mikumi imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya elimu na miundombinu inayotekelezwa katika halmashauri ya jiji la Mbeya na halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya cde: Juma Zuberi Homera ameiambia kamati ya Bunge ya TAMISEMI kuwa kutokukamilika kwa shule ya wasichana ya Mkoa iliyopo Wilayani Kyela ni kutokana changamoto mbalimbali ambazo tayari zimeshawasilishwa kwa Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI mhe Deogratius Ndejembi kwa kushirikiana na mratibu wa miradi SEQIUP ili ziweze kutatuliwa.
Homera ameyasema haya leo tarehe 11/01/2023 baada ya mjumbe kutoka kamati ya Bunge TAMISEMI kuhoji juu ya sababu za kutokakamilika shule hiyo baada ya kuwasili leo ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza Ziara yao ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha amesemamiradi yote ya SEQIUP kwa Mkoa wa Mbeya imetekelezwa vizuri licha ya changamoto hiyo ya shule ya wasichana ambayo nayo si muda inakwenda kutatuliwa.
Baada ya ufafanuzi huo wa Mkuu wa Mkoa Homera, Naibu Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi aliwatoashaka wajumbe na kuahidi kuja nan jia mbadala ya kutatua changamoto hiyo kwa wakati, majibu ambayo yamepokelewa vyema na wajumbe wa kamati
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.