Kamati ya siasa ya wilaya ya Mbeya imefanya ziara ya siku tatu kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri ya wilaya ya Mbeya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)
Kamati ya siasa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ndugu Ackim S. Mwalupindi wametembelea Zahanati ya Idimi iliopo kata ya Ihango na kujionea ujenzi wa Zahanati hiyo ilojengwa kwa nguvu za wananchi na kuwezeshwa umaliziaji na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Aidha kamati imetembelea kuona Barabara ya Isyonje-Kikondo ambayo inatarajiwa kutengenezwa kwa kiwango cha lami katika kata ya Ilungu. Pia kamati ilitembelea kituo cha Afya Ilungu na kukagua jengo la mama na mtoto ambalo tayari limeanza kutumika.
Kituo cha Afya cha Ilungu wamepatiwa gari la kubebea wagonjwa na Mkurugenzi Mtendaji ndugu Stephen E. Katemba kufuatia umbali wa huduma kutoka Ilungu hadi Hospitali kubwa ya Ifisi.
Kamati ya siasa ilitembelea pia shule ya Msingi Shilanga, ni miongoni mwa shule kongwe na yenye ufaulu mzuri,mpango mkakati wa halmashauri ni kukarabati shule kongwe zote za halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kidogo kidogo. Mkurugenzi Mtendaji ametoa ndoo saba za rangi ili kuboresha na kupendezesha shule hiyo.
Pia kamati ilitembelea shamba la parachichi la halmashauri lililopo Itewe, mradi wa ujenzi wa shule tarajiwa ya Sekondari Ihombe,mradi wa nyumba za wakuu wa idara na mradi wa ujenzi wa bweni la Watoto wenye ulemavu liliopo kata ya Nsalala.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.