Halmashauri ya wilaya ya Mbeya yapokea kiasi cha shilingi bilioni 3.51 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, vituo shikizi,ujenzi wa chumba cha huduma za wagonjwa mahututi(ICU),ununuzi wa mashine ya miozi(X-RAY) pamoja na ujenzi wa nyumba za watumishi.
katika fedha hizi shilingi bilioni 1.84 ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 92 katika shule za sekondari, bilioni 1.06 uboresha wa mazingira ya vituo shikizi 26 kwa kujenga madara 53,ujenzi wa chumba cha huduma za wagonjwa mahututi(ICU) kiasi cha shilingi milioni 100 kutumika, ununuzi wa mashine ya miozi kiasi cha shilingi milioni 420 zimepokelewa pamoja na ujenzi wa nyumba za watumishi kiasi cha shilingi milioni 90 zitatumika.
fedha bilioni 3.51 zilizopokelewa katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya ni mkopo kutoka shirika la fedha Duniani (IMF) kwa ajili ya mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19 ili kuboresha mazingira ya kutolea huduma za afya na elimu
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.